Loading...

Kupima UKIMWI ni lazima nchini Zambia

Rais wa Zambia, Edgar Lungu
Rais wa Zambia, Edga Lungu ameamuru kuwa kila raia nchini humo ni lazima apimwe ugonjwa wa ukimwi ili kuliweka taifa katika uwazi kuhusu takwimu za waathirika.

Zambia inatajwa kuwa ni kati ya nchi zenye viwango vya juu zaidi vya maambukizi ya UKIMWI kusini mwa bara la Afrika kwa asilimia 11.6, huku watu walio na umri wa kati ya miaka 15 na 49, wakiwa wanaishi na virusi vinavyosababisha UKIMWI.

Rais Lungu amesema kuwa kupimwa na kupewa ushauri na matibabu sio kitu cha kujitolea, katika jitihada za kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi nchimi humo.
Kupima UKIMWI ni lazima nchini Zambia Kupima UKIMWI ni lazima nchini Zambia Reviewed by Zero Degree on 8/16/2017 11:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.