Loading...

Kauli ya Costa baada ya Chelsea kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Burnley


Mechi ya kwanza ya Chelsea ya ufunguzi wa Ligi Kuu ilikuwa ni ya maumivu kwao kufuatia kichapo cha goli 3-2 wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani ambapo Diego Costa naye alionyesha hisia zake baada ya matokeo hayo.

Katika mahojiano na mwandishi wa 'Daily Mail', Adam Crafton, Costa alitoa maoni yake baada ya mchezo kumalizika.

Wakati ambapo Chelsea ilikuwa tayari imefungwa goli 3-0: "Naona sasa mambo yanaenda vizuri kwa Chelsea, sio?" alihoji kinafiki.


“Lakini pamoja na hayo kadi nyekundu ilibadilisha mchezo kwa ujumla.”


Wakati mchezo ulipokaribia kuisha, baba mzazi wa Costa, Zeinha, aliingilia. Zeinha alitikisa kichwa chake akionekana kurahia matokeo ya Chelsea, ambapo Costa aliitikia kwa kusema: “Baba! Sio haki, kumbuka tayari wana upungufu wa wachezaji wawili.”

Costa pia alikiri kuumizwa na kukosa katika mshikemshike wa Ligi Kuu ya Uingereza:


“Ligi kuu ya Uingereza ndio bora zaidi. Nyakati kama hizi, mtu unapokuwa unakimbizana mchezoni, na ile hali sekunde za kufanya mabadiliko unazo....,” Costa alizungumzia pia juu ya ufunguzi wa Ligi Kuu ya Uingereza. “Tunaishi kwa ajili ya soka. Uliona Arsenal walipocheza dhidi ya Leicester? Baadae Liverpool nao wakipata matokeo ya goli 3-3, dakika ya mwisho! Rooney akiifungia Everton! Nitakuwa mbinafsi kama nitasema sijazikumbuka nyakati hizo.”

Kwa sasa maisha yajayo kisoka kwa Costa bado ni kizungumkuti kufuatia nyota huyo kudai Chelsea inamchukulia kama mhalifu na kutishia kuendelea kubakia na familia yake nchini Brazil hadi pale atakapouzwa.
Kauli ya Costa baada ya Chelsea kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Burnley Kauli ya Costa baada ya Chelsea kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Burnley Reviewed by Zero Degree on 8/16/2017 11:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.