Loading...

Kiasi ambacho Barcelona wamejiandaa kumlipa Messi asiiwazie Manchester City


Barcelona wamejiandaa kumpa Lionel Messi mkataba mnono unaoambatana na pesa ya ziada itakayovunja rekodi atakaposaini mkataba mpya Nou Camp.

Nyota huyo wa Argentina anamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu na bado hajaongeza mkataba wake na klabu hiyo.

Mwezi uliopita, Rais wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu alisisitiza kwamba, kilichobakia ni yeye (Messi) kusaini mkataba baada ya kukubaliana na malipo ya mshahara wa paundi laki tano kwa wiki.

Taarifa ya Gazeti la Catalunya, "L'Ara", inadai kwamba Barcelona watampa Messi kuanzia kati ya paundi milioni 79 hadi 85 kama pesa ya ziada itakayoambatana na mkataba huo.



Baada ya kuipeleka Argentina Kombe la Dunia, Messi sasa anatarajiwa kusaini mkataba huo mwezi Novemba.

Barcelona wanapata jeuri hiyo kufuatia dili jipya walilosaini na kampuni ya Nike na mdhamini wa Maboresho ya Uwanja wa Nou Camp.
Kiasi ambacho Barcelona wamejiandaa kumlipa Messi asiiwazie Manchester City Kiasi ambacho Barcelona wamejiandaa kumlipa Messi asiiwazie Manchester City Reviewed by Zero Degree on 10/12/2017 07:27:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.