Loading...

Timu ya KMC [ Ligi Daraja la Kwanza ] yanasa nyota watano toka ligi kuu.

Athuman Idd Chuji .

Timu ya KMC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza imeonyesha jeuri ya fedha baada ya kunasa nyota watano kutoka timu za Ligi Kuu.

Nyota hao wamepatikana wakati dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa Agosti 8 mwaka huu.

Timu hiyo inayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, msimu uliopita ilimaliza ligi hiyo ikiwa nafasi ya nne kwenye Kundi A nyuma ya African Lyon, Ashanti United na Friends Rangers.

Wachezaji hao ambao KMC imeshawasajili hadi sasa ni Erick Mawala (Mbeya City), Rashid Roshwa na Lambele Jerome (Kagera Sugar), Musa Kidu (JKT Ruvu) na Athuman Iddi ‘Chuji’ (Mwadui).

Kiungo Erick Mawalla aliyesajiliwa kutoka Mbeya City amesema amekoshwa na usajili uliofanywa na KMC akidai utaisaidia timu hiyo kupanda Ligi Kuu.

ZeroDegree.
Timu ya KMC [ Ligi Daraja la Kwanza ] yanasa nyota watano toka ligi kuu. Timu ya KMC [ Ligi Daraja la Kwanza ] yanasa nyota watano toka ligi kuu. Reviewed by Zero Degree on 8/04/2016 10:33:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.