Loading...

Kampuni ya AM Arts Promotion yaja na Kanumba Star Search.

KAMPUNI ya AM Arts Promotion imeandaa programu ya kusaka vijana wenye vipaji vya kuigiza. Programu hiyo itajulikana kwa jina la 'Kanumba Star Search'.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Janet Mwombeki alisema wameamua kuanzisha shindano hilo kwa lengo la kuenzi mchango wa msanii Steven Kanumba katika fani ya maigizo.

"Tunafahamu juhudi kubwa za marehemu Kanumba katika kustawisha sanaa ya filamu ndani na nje ya nchi," alisema Mwombeki.

Aliongeza: "Kwa kutambua hilo, tumeandaa programu hii ili kupata vijana watakaoweza kuendeleza mazuri aliyofanya Kanumba," alisema Mwombeki.

Alisema tayari wameanza msako huo kwa kukusanya vijana kutoka maeneo mbalimbali ambao watapimwa uwezo wao.

"Kikubwa tunaomba wadhamini ili kulifanikisha shughuli hii," alisema Mombeki.


Mama wa Kanumba, Florence Mutegoa, aliishukuru kampuni hiyo kwa kuamua kuwasaidia vijana. 

"Tutashirikiana kuhakikisha kazi hii inafanikiwa. Naziomba kampuni na taasisi kujitokeza kudhamini," alisema Mutegoa.


ZeroDegree.
Kampuni ya AM Arts Promotion yaja na Kanumba Star Search. Kampuni ya AM Arts Promotion yaja na Kanumba Star Search. Reviewed by Zero Degree on 8/04/2016 10:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.