Loading...

Neymar kushuka dimbani leo wakati PSG itakapocheza dhidi ya Guingamp


SUPASTAA wa klabu ya PSG, Neymar, anatarajia kushuka dimbani leo na kucheza mechi yake ya kwanza ya Ligue 1 dhidi ya timu ya Guingamp.

Mchezaji huyo mwenye thamani zaidi duniani ilikuwa awe huru kucheza tangu wiki iliyopita, lakini matatizo ya kibenki yalipelekea asubiri hadi kila kitu kitakapokuwa sawa.

Neymar, 25, alishindwa kucheza mechi ya kwanza ya ligi hiyo dhidi ya Amiens wikiendi iliyopita kutokana na makabrasha ya uhamisho wake kutokamilishwa.

Kwa muda wote huo, Neymar alikuwa akiisubiria ITC yake kutokana na Barca kuizuia kwa madai ya kusubiri fedha zote za uhamisho wake zilipwe.

Fedha hizo tayari zimeshalipwa na ITC ya Neymar imeshawasili mezani kwa Chama cha Soka cha Ufaransa, FFF, ambao wamethibitisha hilo.

PSG itachuana na Guingamp kwenye dimba la Stade du Roudourou usiku wa leo, muda sawa na Barcelona itakapochuana na Real Madrid kwenye dimba la Camp Nou, mchezo wa Spanish Super Cup.
Neymar kushuka dimbani leo wakati PSG itakapocheza dhidi ya Guingamp Neymar kushuka dimbani leo wakati PSG itakapocheza dhidi ya Guingamp Reviewed by Zero Degree on 8/13/2017 03:58:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.