Loading...

Conte ametuma ujumbe wa kukatisha tamaa kwa mashabiki wa Chelsea kuhusu Hazard


Antonio Conte amekiri kwamba hajui ni lini Eden Hazard atakuwa tayari kurejea dimbani kuitumikia klabu ya Chelsea.

Raia huyo wa Ubelgiji hakushiriki kwenye michezo ya awali kabla ya ufunguzi Ligi Kuu kufufatia kuumia wakati akiitumikia timu yake ya taifa kwenye michuano ya kimataifa.

Meneja wa klabu ya Chelsea, muitaliano, Antonio Conte amesema kwamba, hawezi kueleza ni muda gani nyota huyo atakuwa tayari kurejea dimbani na kuungana na wenzake katika kutekeleza majukumu ya klabu.

Alipoulizwa kuhusu Hazard wakati wa mahojiano na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa jana, Conte alijibu: “Ni vigumu sana kutaja muda sahihi au tarehe ya Hazard kurejea. Hakika ni
 vigumu.”


Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 anatarajia kurejea kibaruani ndani ya wiki kadhaa zijazo, na amekua akitia bidii kubwa katika suala zima la kuuweka mwili sawa kwenye kambi ya mazoezi ya klabu ya Chelsea katika majira haya ya joto.
Conte ametuma ujumbe wa kukatisha tamaa kwa mashabiki wa Chelsea kuhusu Hazard Conte ametuma ujumbe wa kukatisha tamaa kwa mashabiki wa Chelsea kuhusu Hazard Reviewed by Zero Degree on 8/13/2017 03:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.