Loading...

Davido ahojiwa na Polisi kufuatia kifo cha rafiki yake wa karibu


Polisi katika mji wa Lagos nchini Nigeria wanasema kuwa wanamchunguza mwanamuziki Davido, ambaye jina lake kamili ni David Adeleke, kufuatia utata unaozunguka kifo cha rafiki yake Tagbo Umeike.


Msemaji wa polisi aliiambia BBC kuwa Davido hajachukuliwa kuwa mshukiwa wakati huu, lakini akathibitisha kuwa mwanamuziki huyo wa afrobeats, aliitwa kuhojiwa pamoja na familia ya Tagbo, ambao walikuwepo wakati wa kifo chake.

Tunachunguza ni wapi Davido alienda, kanda ya video, ili kupata picha wazi kuhusu kile kilichotokea. alisema msemaji huyo.

Bw. Tagbo, rafiki yake Davido alifariki tarehe 3 Oktoba na mwili wake ukaachwa nje ya hospitali mjini Lagos.

Davido amekana kabisa kuhusika kwenye kifo cha rafiki yake.
Davido ahojiwa na Polisi kufuatia kifo cha rafiki yake wa karibu Davido ahojiwa na Polisi kufuatia kifo cha rafiki yake wa karibu Reviewed by Zero Degree on 10/12/2017 07:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.