Loading...

Moto wauwa watu wasiopungua 27

Wazima moto wakizuia moto kusambaa katika eneo lililowaka moto kwenye jengo la makazi ya watu huko Istanbul Aprili 2, 2024.


Moto katika klabu ya starehe ya usiku mjini Istanbul, Uturuki wakati ikifanyiwa ukarabati Jumanne umeuwa watu wasiopungua 27, maafisa na taarifa mbalimbali zimesema.

Watu kadhaa, wakiwemo mameneja wa klabu hiyo, walishikiliwa na polisi kuhojiwa. Wakati huo huo, ofisi ya gavana wa Istanbul ilisema katika taarifa kuwa mtu mmoja anatibiwa hospitali.

Klabu hiyo ya Masquerade, ambayo ilifungwa kwa ajili ya ukarabati, ilikuwa katika jengo lenye ghorofa 16 ya jumba la makazi ya watu katika wilaya ya Besiktas upande wa mji uliotenganishwa na eneo la Bosphorus. Moto huo ulizimwa.

Gavana Davut Gul aliwaambia waandishi wa habari katika eneo la tukio kuwa chanzo cha moto huo kinachunguzwa na waathirika walisadikiwa kuhusika katika shughuli za ukarabati.

Mamlaka imewakamata watu watano kwa ajili ya kuwahoji, wakiwemo mameneja wa klabu hiyo na mtu mmoja aliyekuwa ana jukumu la kufanya ukarabati huo, Waziri wa Sheria Yilmaz Tunc alisema.

Meya Ekrem Imamoglu alisema mamlaka zilikuwa zinakagua jumba kutathmini usalama wake.

Wazima moto kadhaa na timu ya madaktari wamepelekwa katika eneo la tukio hilo, alisema.

Credits: Voa
Moto wauwa watu wasiopungua 27 Moto wauwa watu wasiopungua 27 Reviewed by Zero Degree on 4/03/2024 09:26:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.