Loading...

Kiduku: Hakuna ugomvi rahisi



Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Twaha Kiduku leo Aprili 3,2024 amewaongoza mabondia wenzake mkoani Morogoro kupima afya kuelekea pambano lake dhidi ya Hapreet Sight kutoka India.

Pambano hilo la Kimataifa lisilokuwa la ubingwa lililopewa jina la ‘Hatukimbii Hatuogopi’ linatarajia kupigwa siku ya Idd Pili kwenye ukumbi wa Tanzanite, mkoani Morogoro.

Akizungumzia maandalizi yake, Kiduku amesema amekamilisha kwa asilimia kubwa na yupo tayari kuliwakilisha vizuri Taifa kwa kuibuka na ushindi.

“Mimi pamoja na timu yangu tuko vizuri kiafya na kila kitu, naamini siwezi kuwaangusha Watanzania. Hakuna ugomvi rahisi, siku zote ugomvi ni ugomvi kikubwa ni kujiandaa na kumheshimu mpinzani,” amesema Kiduku.

Mara ya mwisho Kiduku alipanda ulingoni Desemba mwaka jana na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa pointi dhindi ya Mganda, Mohammed Sebyala, jijini Dar es Salaam.

Credits: Mtanzania
Kiduku: Hakuna ugomvi rahisi Kiduku: Hakuna ugomvi rahisi Reviewed by Zero Degree on 4/03/2024 10:26:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.