Loading...

Watoto 4 wafariki nchini Burundi baada ya kanisa kuporomoka


Mvua kubwa iliyonyesha kusini mwa Burundi imesababisha vifo vya watoto wanne baada ya kanisa walimokuwa kuporomoka huku watu wengine 15 wakijeruhiwa siku ya Jumapili, kulingana na afisa wa eneo hilo na vyombo vya habari vya serikali.

Mvua kubwa ikiandamana na upepo mkali ilianza kunyesha Kiyange mwendo wa saa moja asubuhi, afisa wa serikali ya mtaa Esperance Inarukundo aliliambia shirika la habari la AFP.

Hali mbaya ya hewa "ilisababisha uharibifu mkubwa, ikiwa ni pamoja na kuporomoka kwa kanisa la kipentekoste la Kiyange," ambapo watoto walikuwa wakihudhuria madarasa ya elimu ya dini, Inarukundo alisema.

"Tunaendelea na upekuzi kwenye vifusi na tayari tumegundua miili ya watoto wanne waliokufa na majeruhi 15 kanisani," alisema na kuongeza kuwa wakaazi wa eneo hilo, Shirika la Msalaba Mwekundu la Burundi na idara ya ulinzi wa raia walikuwa wakisaidia shughuli ya uokoaji.

Shirika la Habari la Burundi linalomilikiwa na serikali lilithibitisha idadi ya waliofariki kwenye mtandao wa X, uliojulikana zamani kamaTwitter, likisema kuwa "ukuta wa kanisa uliangukia watoto hao.

Burundi ambayo ni nyumbani kwa watu milioni 12, ni moja ya nchi maskini zaidi duniani.
Watoto 4 wafariki nchini Burundi baada ya kanisa kuporomoka Watoto 4 wafariki nchini Burundi baada ya kanisa kuporomoka Reviewed by Zero Degree on 10/15/2023 06:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.