Cameron yaonywa dhidi ya kuishambulia Syria
Serikali ya Uingereza inasema kuwa huenda ikaachana na mpango wa kuomba idhini ya bunge ili kuanzisha mashambulizi ya angani nchini Syria.
Ripoti hizo zilitolewa baada ya kamati ya bunge inayohusika na masuala ya mashauri ya nchi za kigeni kusema kuwa inapinga hatua zozote za kijeshi kutoka nchini Uingereza.
Kamati hiyo inasema kuwa kabla ya mashambulizi ya angani kufanyika, inahitajika kuwepo jitihada za pamoja za kimataifa za kushinda wanamgambo wa kiislamu na kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini syria.
Waandishi wa BBC wanasema kuwa kuna dalili kuwa waziri mkuu wa Uingereza David Cameron hana matumaini kuwa anaweza kupata uungwaji mkono wa kutosha kuweza kupata idhini ya bunge.
Source: BBC
Cameron yaonywa dhidi ya kuishambulia Syria
Reviewed by Zero Degree
on
11/03/2015 06:46:00 PM
Rating: