Loading...

Waangalizi wa uchaguzi TZ waipinga ZEC

Wanachama wa tume ya uchaguzi Zanzibar, ZEC

Waangalizi wa uchaguzi mkuu wa ndani nchini Tanzania TEMCO wamesema kuwa wanashangazwa na hatua ya tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC ya kudai kuwa uchaguzi visiwani humo haukuwa huru na haki.

Mwenyekiti wa TEMCO Dr Bennson Bana anasema kuwa amesema kuwa kwa mjibu wa waangalizi wao waliokuwa katika vituo vitu mbalimbali visiwani humo walijiridhisha na hatua za uchaguzi huo pamoja na kwamba mwisho wa siku uchaguzi huo ukafutiliwa mbali na tume.
Bana pia amesema kuwa TEMCO ilishtushwa na tamko la octoba 26 2015 lililokuwa lililosomeka kuwa CUF yashinda uchaguzi wa kihistoria Zanzibar.
Msimamo wa TEMCO ni kuisihi tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC kufikiria upya umamuzi iliyoufikia,lakini wamevishauri vyama vya siasa Zanzibar kuzingatia katiba na sharia kwa mjibu wa katiba.
Image captionWaangalizi wa uchaguzi mkuu nchi Tanzania
Wakizungumzia uchaguzi wa Tanzania Bara TEMCO wamesema kuwa uchaguzi wa mwaka hu kwa Tanzania bara ulikuwa ni huru na haki na kwamba wapiga kura walijitokeza kwa wingi.
Hata hivyo katika baadhi ya migogoro iliyosalia kutokana na uchaguzi mkuu waangalizi hawa wamewataka wanasiasa kutokuwa chanzo cha uvunjifu wa Amani badala yake wanapaswa kuwa kiungo mhimu katika suala zima la kudumisha Amani.

Source: BBC
Waangalizi wa uchaguzi TZ waipinga ZEC Waangalizi wa uchaguzi TZ waipinga ZEC Reviewed by Zero Degree on 11/03/2015 06:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.