Loading...

Wahariri wa Gazeti la Mawio wajisalimisha Polisi.


Dar es Salaam. Wahariri wa gazeti la Mawio waliokuwa wanatufutwa na Jeshi la Polisi, jana mchana walikwenda Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa.

Wahariri hao walihojiwa kwa muda wa saa nne kuanzia saa 8:59 mchana hadi Saa 12 : 40 jioni.

Wahariri hao ni Jabir Idrisa na Saimon Mkina ambaye aliongozana na Frederick Kihwelo, ambaye ni mwawanasheria wa gazeti hilo, Absalom Kibanda (mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri), Saed Kubenea (mkurugenzi wa kampuni ya Halihalisi Publishers) na Ansbert Ngurumo, aliyekuwa mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima.

Januari 15, kamanda polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwataka wahariri hao kujisalimisha kituoni hapo, akidai kuwa wameandika habari za uchochezi.

Mapema jana kabla ya kuwasili kwa wahariri wa gazeti hilo, Kamanda Sirro alidai kuwa wamekuwa wakiwatafuta bila ya mafanikio.

Wakati Idrisa anaingia ofisi ya Kamanda Sirro kwa ajili ya mahojiano, waandishi walizuiwa, waliambiwa hawahusiki, baadaye saa 9:15 alasiri Mkina aliwasili na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi hiyo, lakini alitakiwa asubiri nje.

“Sisi jukwaa la wahariri hatutakubali kufanya kazi na waziri wa aina hii na tutatoa tamko ngojeeni,”alisema Kibanda baada ya kufika kituoni hapo.

Kwa upande wake Kubenea alisema alifika hapo kwa sababu miongoni mwa walioshikiliwa na polisi ni mfanyakazi wake.


ZeroDrgree.
Wahariri wa Gazeti la Mawio wajisalimisha Polisi. Wahariri wa Gazeti la Mawio wajisalimisha Polisi. Reviewed by Zero Degree on 1/19/2016 12:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.