Loading...

Operesheni ya kuzuia viroba nchini iko pale pale, Waziri Makamba

Serikali imesisitiza kuwa operesheni ya kukagua usitishaji wa utengenezaji , uuzaji na matumizi ya pombe zinazofungashwa katika mifuko ya plastiki 'viroba' ipo pale pale na itaanza Machi 2 mwaka huu.
Msisitizo huo umetolewa leo (Jumanne) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam. 

Kabla ya Makamba kutoa msisitizo huo ikiwa ni mara ya pili leo, Februari 16 mwaka huu, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitangaza Serikali kupiga marufuku pombe ifikapo hizo Machi Mosi mwaka huu.

Makamba amesema katika operesheni ya kukagua viroba itakuwa nchi nzima na itaendeshwa na kamati za ulinzi na usalama na kamati za mazingira katika ngazi ya mkoa, wilaya,tarafa , kata na vijiji.

"Ukikutwa unakunywa, unauza na utengeneza au kuingiza viroba utachukuliwa hatua kali zikiwamo faini na kifungo au vyote kwenda sambamba," amesema Makamba.

Source: Mwananchi
Operesheni ya kuzuia viroba nchini iko pale pale, Waziri Makamba Operesheni ya kuzuia viroba nchini iko pale pale, Waziri Makamba Reviewed by Zero Degree on 2/28/2017 01:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.