Loading...

Viroba sasa kupigwa marufuku rasmi nchini Tanzania kuanzia Tar 1 ya mwezi Machi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuanzia Machi Mosi, mwaka huu Serikali itapiga marufuku pombe kali maarufu kwa jina la ‘viroba’.

Ametoa kauli hiyo wakati akizumgumza na maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara.

“Tumekaa na wenye viwanda na kukubaliana kuwa wanaotengeneza Pombe waziweke katika ukubwa unaokubalika. sasa hivi viroba vimeenea kila kona hata watoto wa shule za msingi wanatumia kwa sababu ni rahisi kuweka mfukoni na kutembea navyo. Kuanzia tarehe moja Machi, tutakayemkamata ameshika pombe ya viroba, sisi na yeye.”

Hivi karibuni bunge lilijadili suala la usitishaji wa pombe aina ya hiyo na kuahidi lipo katika mchakato.
Viroba sasa kupigwa marufuku rasmi nchini Tanzania kuanzia Tar 1 ya mwezi Machi Viroba sasa kupigwa marufuku rasmi nchini Tanzania kuanzia Tar 1 ya mwezi Machi Reviewed by Zero Degree on 2/17/2017 06:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.