Loading...

Waziri amewataka wananchi kuwa makini na matangazo ya ajira yanayozagaa mitaani

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu Mh.JENISTA MHAGAMA amewatahadharisha wananchi kuwa makini na Mabango ya ajira yanayozagaa barabarani.

Waziri Mhagama ametoa tahadhari hiyo alipokuwa akizungumzia Mada kuhusu kuwepo kwa utitiri wa Mabango ya Ajira yanayoambatana na ahadi za uongo kwenye Mishahara.

Mh. Mhagama amesema wizara yake itahakikisha inashirikian ana mamlaka husika hasa halimashauri na manispaa zote nchini kuona uhalali wa mabango hayo na kwamba hatua zitachukuliwa kwa watakaobainika kukiuka sheria za ajira.

kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam ISAYA MWITA amesema kuwa utaratibu wa kuweka Mabango upo kisheria katika Halmashauri ila usumbufu mkubwa ni kuwa matangazo madogo madogo ambayo mengi yanawekwa kwenye karatasi za A4 ambayo yanabandikwa kwenye kuta za nyumba, nguzo za umeme na miti.

Amebainisha kuwa wapo katika mchakato wa kukutana na viongozi wa jiji wakiwemo Madiwani, Wenyekiti wa Halmashauri na wengine ili kuweka utaratibu wa kudhibiti matangazo hayo, ikiwemo kuweka sheria ndogo ndogo lengo likiwa ni kuwapunguzia kero wananchi ambao wanaumizwa na matangazo hayo.
Waziri amewataka wananchi kuwa makini na matangazo ya ajira yanayozagaa mitaani Waziri amewataka wananchi kuwa makini na matangazo ya ajira yanayozagaa mitaani Reviewed by Zero Degree on 3/02/2017 03:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.