Loading...

Mkemi agomea wito wa kamati ya nidhamu ya TFF

Baada ya Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) kumshitaki kwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa klabu ya Yanga, msemaji huyo Salum Mkemi, amesema kuwa hatofika kusikiliza shitaka lake kwani ana majukumu ya timu yake ambayo inajiwinda na Mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya wafalme wa Misitu, Klabu ya Mbao Fc.

Mkemi alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo kesho Jumapili katika Ofisi za shirikisho, mapema saa 5 asubuhi baada ya kushutumiwa kwa kuidhalilisha Kamati ya Saa 72, kuwa inaendeshwa kwa unazi na imegubikwa na rushwa katika kulishughulikia suala la kadi tatu za njano kwa mchezaji, Mohammed Fakhi wa klabu ya Kagera Sugar.

Mkemi amesema: “Sitaweza kwenda kusikiliza nilichoitiwa katika siku hiyo ya Jumapili kwani nipo Mwanza na timu na ndiyo kiongozi wa msafara.

“Tunacheza na Mbao hiyo Jumapili hivyo nimeandika barua kwa TFF kuwataarifu kuwa sitoweza kufika siku hiyo kama kamati ilivyonitaka hivyo wanipangie siku nyingine.

“Mimi sio mhalifu isipokuwa ni tuhuma tu juu yangu, hivyo nitakapopangiwa siku nyingine nitakwenda, na wamekubali ombi langu hilo.”

Juzi, Wambura alitoa taarifa ya Mkemi kutakiwa kwenda kujieleza mbele ya Kamati ya Nidhamu kwa kosa la kuishambulia Kamati ya Saa 72.
Mkemi agomea wito wa kamati ya nidhamu ya TFF Mkemi agomea wito wa kamati ya nidhamu ya TFF Reviewed by Zero Degree on 4/29/2017 02:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.