Vikao vya Bunge vyasitishwa ili kuuaga mwili wa Marehemu Elly Macha [Chadema]
Katika kile kilichoonekana kuwa ratiba za kawaida za bunge zisiharibike Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Job Ndugai alieleza wabunge jana kuwa bajeti ya TAMISEMI na ile ya Ofisi ya Raisi Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora majadiliano yalitakiwa yamalizike jana hiyo hiyo ili leo shughuli za kuuga mwili wa Dkt. Macha ziweze kufanyika.
Agizo hilo la Spika wa Bunge lilitekelezeka jana hiyohiyo ambapo bunge liliweza kuhitimisha bajeti ya ofisi hizo za rais majira ya saa tatu usiku.
Agizo hilo la Spika wa Bunge lilitekelezeka jana hiyohiyo ambapo bunge liliweza kuhitimisha bajeti ya ofisi hizo za rais majira ya saa tatu usiku.
Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameongoza waombolezaji kuaga mwili wa Marehemu Dkt Elly Marko Macha Mbunge wa Viti Maalum-CHADEMA katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Dkt. Macha alifariki dunia Machi 31, 2017 katika Hospitali ya New Cross nchini Uingereza alikokuwa akitibiwa.
Macha aliyekuwa mlemavu wa macho tangu akiwa mtoto wa miezi mitano, amefariki akiwa na umri wa miaka 55 (1962-2017).
Baada ya kuaga mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda nyumbani kwake Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Vikao vya Bunge vyasitishwa ili kuuaga mwili wa Marehemu Elly Macha [Chadema]
Reviewed by Zero Degree
on
4/21/2017 12:50:00 PM
Rating: