Loading...

Deus Kaseke, Msuva na Chirwa wamesimamishwa Ligi Kuu Bara na Kamati ya saa 72

Kamati ya Saa 72 imekaa kupitia mambo mbalimbali na moja ya uamuzi wake ni kuhusiana na wachezaji wa Yanga kumuangusha mwamuzi wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC na imeamua kuwasimamisha kuitumikia Ligi Kuu Bara.

Wachezaji Deus Kaseke, Simon Msuva na Obrey Chirwa wa Yanga wamesimamishwa kucheza mechi za Ligi Kuu wakati wakisubiri suala lao la kumsukuma na kumwangusha Mwamuzi Ludovic Charles kusikilizwa na kutolewa uamuzi na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Walifanya kitendo hicho katika mechi hiyo dhidi ya Mbao FC iliyofanyika Mei 20, 2017 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijni Mwanza. Uamuzi wa Kamati umezingatia Kanuni ya 9(5) ya Ligi Kuu.

Mwamuzi Ludovic Charles amepewa onyo kali kwa kutodhibiti vizuri mchezo. Uamuzi dhidi yake ni kwa mujibu wa Kanuni ya 38(5) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
Deus Kaseke, Msuva na Chirwa wamesimamishwa Ligi Kuu Bara na Kamati ya saa 72 Deus Kaseke, Msuva na Chirwa wamesimamishwa Ligi Kuu Bara na Kamati ya saa 72 Reviewed by Zero Degree on 5/26/2017 02:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.