Loading...

Majeruhi wawili wa ajali ya Lucky Vincent wameruhusiwa kutoka hospitali

Mjumbe wa Baraza la Congress la Marekani, Steve King-R (aliyechuchumaa) akizungumza na mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Lucky Vincent, Doreen Mshana anayetibiwa katika Hospitali ya Mercy iliyopo Jiji la Sioux. Steve alikwenda kuwajulia hali wanafunzi watatu wa shule hiyo walionusurika katika ajali iliyotokea wilayani Karatu mkoani Arusha na kuua wanafunzi 32, walimu wawili na dereva. Kulia ni daktari bingwa, Steve Meyer. Picha kwa hisani ya Hospitali ya Mercy.
Watoto wawili majeruhi wa ajali ya gari la Shule ya Lucky Vincent wameruhusiwa kutoka hopitalini.

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwa watoto hao, Sadia Ismael na Wilson Tarimo waliokuwa wamelazwa katika hospitali ya Mercy ya Marekani wameruhusiwa na sasa wapo katika makazi mapya.

“Watoto Sadia na Wilson waruhusiwa rasmi kutoka hospitali ya Mercy na wanaelekea kwenye makazi yao mapya mjini Sioux City IA. Mungu azidi kuwaangazia nuru ya uso wake. Amani iwe nawe na Nesi wetu mpendwa kwa huduma kubwa mmefanya kwa watoto hawa na Tanzania,” ameandika Nyalandu. 

Jana Nyalandu aliandika kuwa mtoto Doreen ataendelea kuwepo hospitali katika wodi ya watoto akiendelea kupata huduma za karibu hadi itakapoamuliwa vinginevyo.
Majeruhi wawili wa ajali ya Lucky Vincent wameruhusiwa kutoka hospitali Majeruhi wawili wa ajali ya Lucky Vincent wameruhusiwa kutoka hospitali Reviewed by Zero Degree on 5/26/2017 10:11:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.