Halima Mdee, Ester Bulaya waingia matatani tena
Mdee (Kawe) na Bulaya (Bunda Mjini), walisimamishwa Juni 5, mwaka huu, baada ya kutuhumiwa kudharau kiti cha Spika.
Ndugai alitoa tahadhari hiyo jana mchana wakati akiahirisha kikao cha Bunge na kutoa matangazo mbalimbali kama ilivyo kawaida.
Akizungumza bila kuwataja majina wabunge hao, Ndugai alisema kuna wabunge waliosimamishwa kwa makosa mbalimbali, lakini nje wanaendelea kulumbana na Bunge kwa kutumia lugha zisizofaa.
Alisema wabunge hao wamekuwa wakitumia lugha za kuudhi dhidi ya Bunge na aliwaonya kuwa ni heri wakaacha kabla hawajachukuliwa hatua kali zaidi.
Aidha, Ndugai alisema anatoa onyo la jumla na la mwisho kwa wabunge hao huku akiwataka ndugu na jamaa wa wabunge hao wawasihi waache kwani wakiendelea zaidi yanaweza kuwapata makubwa.
Wabunge hao wamefungiwa kuhudhuria Vikao vyote vilivyobaki vya Bunge hili kwa mujibu wa adhabu waliyopewa wabunge hao watakuwa nje ya Bunge mpaka Aprili mwaka 2018.
Bulaya na Mdee walisimamishwa baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Newala (CCM), George Mkuchika, kutoa taarifa ya makosa yao bungeni.
Azimio hilo la Bunge lilifikiwa baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Juliana Shonza (CCM), kutoa hoja ya kubadilisha azimio lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge.
Awali, kamati hiyo ilikuwa imependekeza wabunge hao wasihudhurie vikao vya Mkutano huu wa Saba vilivyobaki na vikao vyote vya mkutano wa nane isipokuwa kikao cha siku ya mwisho ya mkutano huo.
Akitoa hoja hiyo, Shonza alisema wabunge hao wawili walipaswa kuwa mstari wa mbele katika kutii maelekezo na masharti mbalimbali yanayotolewa na kanuni za Bunge kwa kuwa wao ni waelewa wa kanuni hizo.

“Nawashauri waache maana kama kuwavumilia tumeshawavulia sana, kama wataendelea wajue kuwa huko huko waliko tuna mamlaka ya kuwaita hapa na kuwapa adhabu kali zaidi ya ile tuliyowapa,” alisema Ndugai.
Aidha, Ndugai alisema anatoa onyo la jumla na la mwisho kwa wabunge hao huku akiwataka ndugu na jamaa wa wabunge hao wawasihi waache kwani wakiendelea zaidi yanaweza kuwapata makubwa.
“Hili ni onyo la jumla jumla na ndugu na jamaa zao ni vizuri wakawaambia waache kutumia lugha ambazo si nzuri kwa Bunge, maana wanaitisha mikutano huko na kusema wanayotaka nasema waache,” alisema Spika Ndugai.
Wabunge hao wamefungiwa kuhudhuria Vikao vyote vilivyobaki vya Bunge hili kwa mujibu wa adhabu waliyopewa wabunge hao watakuwa nje ya Bunge mpaka Aprili mwaka 2018.
Bulaya na Mdee walisimamishwa baada ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Newala (CCM), George Mkuchika, kutoa taarifa ya makosa yao bungeni.
Azimio hilo la Bunge lilifikiwa baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Juliana Shonza (CCM), kutoa hoja ya kubadilisha azimio lililotolewa na Kamati ya Bunge ya Haki,Maadili na Madaraka ya Bunge.
Awali, kamati hiyo ilikuwa imependekeza wabunge hao wasihudhurie vikao vya Mkutano huu wa Saba vilivyobaki na vikao vyote vya mkutano wa nane isipokuwa kikao cha siku ya mwisho ya mkutano huo.
Akitoa hoja hiyo, Shonza alisema wabunge hao wawili walipaswa kuwa mstari wa mbele katika kutii maelekezo na masharti mbalimbali yanayotolewa na kanuni za Bunge kwa kuwa wao ni waelewa wa kanuni hizo.
"Hata hivyo, mara zote kunapotokea fujo hapa bungeni ,Mheshimiwa Halima Mdee na Mheshimiwa Ester Bulaya hawakosekani na wameshawahi kuadhibiwa na Bunge hili kwa vitendo vya utovu wa nidhamu na kudharau Mamlaka ya Spika, hawa tunasema ni wazoefu wa makosa kama haya," alisema Shonza.
Halima Mdee, Ester Bulaya waingia matatani tena
Reviewed by Zero Degree
on
6/14/2017 10:25:00 AM
Rating: