Loading...

Ushirikina: Wanaume wenye vipara wamegeuka dili nchini Msumbiji


Polisi nchini Musumbiji wameonya kuwa wamaume wenye vipara huenda wakalengwa kwenye mashambulizi yanayohusiana na uchawi baada ya kuuliwa kwa wanaume wawili kama hao mwezi uliopita.

Wanaume hao wawili wenye vipara ambapo mmoja alipatikana akiwa amekatwa kichwa na viungo vya mwili vikiwa vimetolewa, waliuliwa katika mkoa wa Zambezia.

"Mwezi uliopita mauaji ya watu wawili wenye vipara yalisababisha kukamatwa washukiwa wawili," msemaji wa polisi Inacio Dina alisema kwenyr mkutano wa waandishi wa habari mjini Maputo.

Mwandishi wa BBC mjini Maputo anasema kuwa baadhi ya watu wana imani potovu kuwa watu wenye vipara wako dhahabu kwenye vichwa vyao.

Visa vya kuuliwa watu wenye vipara kwa uchawi havijaripotiwa siku za nyuma.

Washukiwa ni vijana wa Msumbiji waliowaambia polisi kuwa viungo hivyo vingetumiwa kwa uchawi nchini Tanzania na Malawi.
Ushirikina: Wanaume wenye vipara wamegeuka dili nchini Msumbiji Ushirikina: Wanaume wenye vipara wamegeuka dili nchini Msumbiji Reviewed by Zero Degree on 6/07/2017 03:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.