Diwani mwingine wa Chadema ajiuzulu na kujiunga na CCM
Diwani huyo amekuwa ni wa saba kujiuzulu ndani ya mwezi mmoja katika jimbo la Arumeru Mashariki na Jimbo la Arusha Mjini, Majimbo ambayo wabunge wake ni Joshua Nassari na Godbless Lema wa CHADEMA.
Bw. Jackson amewasilisha barua yake ya kuhama CHADEMA kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Meru, Christopher Kazeri na kutangaza kumuunga mkono Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Ameeleza kwamba, ameamua kujiondoa CHADEMA, baada ya kujiridhisha kuwa kazi ambazo walipanga kufanya kama wapinzania sasa zote zinafanywa na Rais Magufuli hivyo ameamua kumuunga mkono Rais huyo.
Diwani huyo ni wa sita kujiuzulu katika jimbo la Arumeru Mashariki, ambapo katika uchaguzi mkuu uliopita CHADEMA ilishinda viti 25 na CCM kuambulia kiti kimoja pekee
Diwani mwingine wa Chadema ajiuzulu na kujiunga na CCM
Reviewed by Zero Degree
on
7/13/2017 09:10:00 AM
Rating: