Loading...

Man United imetajwa kuwa Klabu ya soka yenye Thamani kubwa zaidi Duniani


Manchester United wanakaa tena kileleni katika ulimwengu wa soka kwa kutajwa kuwa klabu yenye thamani kubwa zaidi duniani.

Hiyo ni kwa upande wa kifedha. lakini inaonekana, Jose Mourinho bado ana kazi kuwa ya kufanya pale Old Traford ili kuweka Manchester katika hali yake ya zamani.

Nje ya uwanja Mashetani hao wekundu wanatajwa kuwa ndio wenye thamani kubwa zaidi duniani kwa mujibu wa gazeti la Forbes, na kuwapita mafundi wa Ligi ya Spain, Barcelona na Real Madrid kwa kuwa na thamani inayokadiliwa kuwa sawa na paundi bilioni 2.85.

Kiasi hicho kimeongezeka kwa asilimia 11%, ongezeko kubwa pekee katika 10 bora, na wamekuwa katika nafasi ya tatu katika klabu zenye thamani kubwa zaidi duniani.

'Dallas Cowboys' wameshirikia nafasi ya kwanza kwa kuwa na thamani zaidi duniani kwa kuwa na thamani ya paundi bilioni 3.25 na nafais ya pili ikijazwa na 'Major Leaguae Baseball's New York Yankees' wenye thamani ya paundi bilioni 2.86
.

Hapo chini ni muonekano wa 10 bora za klabu zote za michezo ikiwa na NFL, MLB, NBA na ulimwengu mzima wa soka kutokea katika nafasi za 50 bora.

Klabu 4 za Ligi Kuu ya Uingereza, Manchester City wakiwa katika nafasi ya 35 kwa thamani ya paundi bilioni 1.61
, Arsenal katika nafasi ya 43 kwa kuwa na thamani ya paundi bilioni 1.49 na Chelsea kushika nafasi ya 45 kwa kuwa na thamani ya paundi bilioni 1.42. Bayern Munich ilikuwa klabu nyingine pekee kutokea katika nafasi za 50 bora wakishikiria nafasi ya 15 kwa kuwa na thamani sawa na paundi bilioni 2.10.

Orodha ya Klabu 10 Bora toka Gazeti la Forbes’ 

1. Dallas Cowboys – 
£3.25 billion
2. New York Yankees – 
£2.86 billion
3. Manchester United – 
£2.85 billion
4. Barcelona – 
£2.82 billion
5. Real Madrid – 
£3.58 billion
6. New England Patriots – 
£2.77 billion
7. New York Knicks – 
£2.55 billion
8. New York Giants – 
£2.40 billion
9. San Francisco 49ers – 
£2.32 billion
10. Los Angeles Lakers – 
£2.32 billion

15. Bayern Munich – 
£2.10 billion
35. Manchester City – 
£1.61 million
43. Arsenal – 
£1.49 billion
45. Chelsea – 
£1.42 billion
Man United imetajwa kuwa Klabu ya soka yenye Thamani kubwa zaidi Duniani Man United imetajwa kuwa Klabu ya soka yenye Thamani kubwa zaidi Duniani Reviewed by Zero Degree on 7/13/2017 07:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.