Batshuayi amjibu Eden Hazard
Mbelgiji huyo aliifungia Chelsea goli la ushindi kwenye Ligi ya Mabingwa dhidi ya klabu ya Atletico Madrid, ambapo Chelsea waliibuka na ushindi wa goli 2-1 ugenini.
Batshuayi ameweka wazi kwamba, Eden Hazard alimshauri abakie na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Batshuayi ameweka wazi kwamba, Eden Hazard alimshauri abakie na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza.
“Ulikuwa ni ushauri unaofaa,” Batshuayi alisikika akiiambia ESPN.
“aliposema hivyo, alidhania kuna uwezekano wa kuwasili kwa mshambuliaji mwingine, lakini mwisho wa siku, tupo wawili tu katika nafasi moja.
“Ninataka kufanikiwa nikiwa ndani ya klabu hii na uhusiano wangu na Morata ni mzuri.
“Sitaki kuondoka mwezi Januari, kwa sababu tunaelekea kucheza michezo mingi na nina uhakika wa kupata nafasi ya kutosha.”
Batshuayi amjibu Eden Hazard
Reviewed by Zero Degree
on
10/06/2017 01:26:00 PM
Rating:
