Neymar: Huu ni "Unyama"
![]() |
Wachezaji wa Brazil wakipata hewa ya oksijeni baada ya sare ya 0-0 dhidi ya Bolivia |
![]() |
Neymar, pia alilamikia mazingira ya uwanja na mpira uliotumika |
Mshambuliaji huyo wa PSG ambaye ndiye mchezaji ghali zaidi duniani kwa sasa alisema "kila kitu kilikuwa vibaya" uwanjani na timu ilikuwa na furaha kwa kuweza kuondoka La Paz na pointi moja.
Neymar alipost kwenye ukurasa wake Instagram: "Sio ubinadamu kucheza katika hali ile, ....uwanja wa vile, mpira wenyewe na hali kadharika kwenye mwinuko kama ule ...kila kitu kilikuwa kibaya. Lakini pamoja na yote hayo, tulikuwa na furaha kwa kiwango tulichokionyesha."
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Tite, ambaye ameifikisha Brazili katika nafasi ya kwanza kwenye kundi lao, alisema: "Lazima niawasifie wataalamu wetu kwa mipango yote iliyofanyika katika idara ya afya ambayo ilitoa msaada mkubwa kuwafanya wachezaji wasiteseke sana na mazingira yale.
"Kiwango kilikuwa cha kushangaza kwani, siku huwa ni vigumu sana kuchezea hapa. Ninafurahia kiwango kilichoonyeswa lakini sikupendezwa na matokeo ya mchezo."
Neymar: Huu ni "Unyama"
Reviewed by Zero Degree
on
10/06/2017 02:07:00 PM
Rating:
