Taarifa mpya kuhusu majeraha ya N'Golo Kante
Kante alipata majeraha nyuma ya goti wakati akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa, na alitegemewa kukosa michezo kadhaa ukiwemo ule wa Manchester United utakaochezwa tarehe 5, Novemba.
Hata hivyo, Conte amesema vipimo vimeonyesha kwamba hali ya Kante sio mbaya kama ilivyokuwa awali na anaweza kurejea uwanjani ndani ya wiki mbili zijazo.
Akizungumza na wwandishi wa habari, Conte alisema: “Natumaini ya kwamba, Kante atarudi kabla ya mapumziko kupisha michuano ya kimataifa, anaendelea vizuri, ....vipimo vimetoa majibu mazuri zaidi ya mwanzo. N'Golo Kante tayari ameanza kufanya mazoezi madogo madogo kujiweka sawa.
“Anaweza kuwa chaguo kwenye mchezo dhidi ya Roma au Manchester United. Kama atakuwepo nitafurahi sana.”
Cesc Fabregas ndiye kiungo pekee kwa Chelsea anayetegemewa kwenye mechi yao dhidi ya Watford wikendi hii.
Taarifa mpya kuhusu majeraha ya N'Golo Kante
Reviewed by Zero Degree
on
10/21/2017 10:05:00 AM
Rating: