Loading...

Conte awatoa hofu mashabiki wa Chelsea


Meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte amepuuzia madai ya kwamba kuna mtafaruku katika klabu hiyo kutokana na mfumo wake wa mazoezi.

Taarifa zimekuwa zikisema wachezaji wa klabu hiyo wamechoshwa na mazoezi makali wanayolazimishwa kuyafanya na kocha wao.

Hata hivyo, Mwitaliano huyo amesema mazoezi anayowafanyisha msimu huu ni asilimia 70% chini ya mazoezi aliyowafanyisha msimu uliopita ambapo Chelsea walinyakua kikombe cha Ligi Kuu ya Uingereza.

"Sina habari kuhusu haya," amesema meneja wa Chelsea Conte, alipoulizwa kuhusu uvumi huo kwenye vyombo vya habari.

Chelsea wamecheza mechi tatu bila kushinda hata moja katika mechi zao za hivi karibuni.

Walishindwa na Manchester City na Crystal Palace kwenye Ligi Kuu kabla ya kutoka sare 3-3 nyumbani dhidi ya Roma Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumatano.

Jumamosi, Chelsea, ambao wako nyuma kwa alama tisa kutoka viongozi wa Ligi Kuu ya Uingereza, Manchester City, watakuwa wenyeji wa Watford na itakuwa ni mechi yao ya tatu ndani ya siku saba.

Conte anaamini kucheza mechi nyingi - pamoja na kukosa muda wa kujiandaa - vimechangia kudorora kwa uchezaji wao.

"Unapocheza kila siku tatu ni vigumu kufanyia kazi mbinu zako za kiufundi na pia hali ya wachezaji," ameongeza.

"Nafikiri sasa hatuangazii zaidi uchezaji kwa kina."

Alipoulizwa iwapo anahisi presha, Conte ameongeza: "Nafikiri kila kocha, kila meneja lazima ahisi presha.

"Ninapokwenda nyumbani kwangu huwa nina furaha kwa sababu najua kila wakati huwa najitoleza kabisa katika kazi yangu kwa klabu hii, mashabiki na wachezaji wangu.

"Lakini mwajua vyema kwamba lolote laweza kutokea katika soka."
Conte awatoa hofu mashabiki wa Chelsea Conte awatoa hofu mashabiki wa Chelsea Reviewed by Zero Degree on 10/20/2017 11:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.