Loading...

Shule 10 bora zilizofanya vizuri kitaifa matokeo ya Darasa la 7

Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde
Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta), limetangaza matokeo ya wa darasa la saba leo ambapo shule bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo ni kama zifuatazo St. Peters – Kagera, St Severine – Kagera, Alliance – Mwanza, Sir. JohnTanga Palikas – Shinyanga, Mwanga – Kagera, Hazina – Dar es salaam, St. Anne Marie – Dar es salaam, Rweikiza – Kagera, Martin Luther – Dodoma.


Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80 .

Sambamba na matokeo hayo pia Dkt. Msonde ametaja ambapo Mikoa 10 iliyoongoza kitaifa ni mkoa wa Dar es salaam , Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, Katavi, Tabora.

Shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa ambazo ni Nyahaa – Singida, Bosha – Tanga, Ntalasha – Tabora, Kishangazi – Tanga, Mntamba – Singida, Ikolo – Singida, Kamwala – Songwe, Kibutuka – Lindi, Mkulumanzi – Tanga, Kitwai A – Manyara.
Shule 10 bora zilizofanya vizuri kitaifa matokeo ya Darasa la 7 Shule 10 bora zilizofanya vizuri kitaifa matokeo ya Darasa la 7 Reviewed by Zero Degree on 10/20/2017 11:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.