Loading...

Kesi ya Lulu yaahirishwa baada ya kukosekana kwa shahidi


KESI inayomkabili muigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, anayedaiwa kumuua muigizaji mwenzake, Steven Kanumba, bila kukusudia, iliendelea leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na kuahirishwa baada ya shahidi upande wa utetezi kutofika mahakamani.

Akiwasilisha maombi, wakili anayeongoza upande wa utetezi, Peter Kibatala, aliiomba, mahakama kupokea ushahidi wa maandishi kwa madai kuwa shahidi aliyeandika maelezo hayo ambaye ni askari polisi wa kituo cha Oyster Bay, Sajenti Nyangea, yuko nje nchi.

Baada ya maelezo hayo ya Kibatala, kulitokea mvutano mkali mahakamani hapo kati ya upande wa Jamhuri na upande wa utetezi ambapo Jamhuri ilikataa kupokelewa ushahidi huo kwa madai kuwa mahakama haiwezi kupokea ushahidi wa maandishi wakati aliyeuandika hayupo.

Aidha Wakili wa Serikali, Faraja George, alimtaka Kibatala asijivishe kofia mbili (wakili na shahidi wa Lulu) kwa kutaka kusoma ushahidi huo mahakamani. Jaji Rumanyika anayesikiliza kesi hiyo alikataa kupokea ushahidi huo na kuiahirisha kesi hadi Oktoba 25 mwaka huu.
Kesi ya Lulu yaahirishwa baada ya kukosekana kwa shahidi Kesi ya Lulu yaahirishwa baada ya kukosekana kwa shahidi Reviewed by Zero Degree on 10/24/2017 02:11:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.