Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 24 Octoba, 2017


Victor Lindelof kupewa kipaumbele kwenye mechi ya Carabao dhidi ya Swansea
ili atetee nafasi yake ndani ya Manchester United.

West Ham wanamtaka kocha wa Hoffenheim, Julian Nagelsmann aje kuwa mrithi wa Slaven Bilic (Star)

Everton wanatazamia kumsajili aliyekuwa meneja wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel kuwa meneja wao mpya baada ya Koeman kutimuliwa.

Philippe Coutinho anasistiza kwamba, timu yote ya Liverpool inastahili kubeba lawama kufuatia kichapo cha goli 4-1 dhidi ya Tottenham.

Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wanahisi Mourinho amevuka mipaka kwa kitendo cha kuwatupia lawama mbele ya vyombo vya habari Jumamosi.

Arsenal, Real Madrid zaingia vitani kusaka saini ya nyota wa Brazil, Alan Guimaraes.

Liverpool watajaribu kumnasa nyota wa Paris Saint-Germain, Julian Draxler mwezi Januari kuziba pengo la Philippe Coutinho (Daily Mirror)

Wachezaji wa Chelsea wamekua wakiwasiliana kwa siri na aliyekuwa kocha wao msaidizi, Steve Holland kwa sababu ya kutokuwa na mahusiano mazuri na Antonio Conte.

Everton wanamtaka Carlo Ancelotti kama meneja wao mpya, lakini muitaliano huyo anamtaka meneja wa Swansea, Paul Clement kuwa kama msaidizi wake.
Jose Mourinho alitupa koti lake sakafuni kwa hasira mbele ya wachezaji wake baada ya kichapo cha Huddersfield.

Jose Mourinho anamvizia nyota wa klabu ya Valencia, Carlos Soler katika dirisha dogo mwezi Januari kwa ofa ya paundi milioni 30.

Manchester City wamemweka Mouctar Diakhaby kwenye orodha ya wachezaji watakaowasajili mwezi januari (Sun)

West Ham wako kwenye mgogoro na wamiliki wa Uwanja wao ulioko London, nchini Uingereza.

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amemhakikishia Jack Wilshere nafasi katika kikosi cha timu hiyo

Zinedine Zidane amemtaja Cristiano Ronaldo kuwa mchezaji wa pekee baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora kwa mara nyingine tena Londdon (Daily Mail).
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 24 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 24 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/24/2017 09:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.