Maneno ya Mourinho kwa wachezaji wake baada ya kufungwa na Huddersfield
Matokeo hayo yanaifanya Manchester City ibakie kileleni kwa tofauti ya ointi tano mbele ya Manchester United.
Mourinho aliwaweka kitimoto wachezaji wake ndani ya chumba cha kubadilishia nguo kufuatia kichapo cha goli 2-1 toka kwa Huddersfield.
Aliwaambia wachezaji wake wawaeleze mashabiki ni kwanini walishindwa kupata matokeo mazuri na ni kwanini walikuwa chini ya kiwango.
Hata hivyo, hakuna mchezaji yeyote aliyekuwa na jibu, si tu kwa Mourinho, bali hata kwa mashabiki wao. Lakini kwa jinsi Tottenham na Chelsea zinavyoifukuzia nafasi yao kwa nyuma, United watatakiwa kutafuta sababu haraka ili kuikaribia Manchester City kileleni.
Sasa Mourinho atakua anatazamia jinsi ya kubabiliana na Tottenham wikendi ijayo kufuatia dozi ya goli 4-1 ambayo Spurs waliitoa kwa Liverpool Anfield wikendi iliyopita.
Maneno ya Mourinho kwa wachezaji wake baada ya kufungwa na Huddersfield
Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2017 12:11:00 PM
Rating: