Loading...

Kichuya awekwa sokoni


UONGOZI wa Klabu ya Simba SC umemuweka sokoni kiungo mshambuliaji, Shiza Kichuya kwa kukaribisha ofa kutoka klabu yoyote.

Hivi karibuni Klabu ya Ismailia ya Misri ilishindwa kufikia makubaliano na Simba juu ya dau la kumsajili kiungo huyo ambalo lilikuwa dogo, na kupelekea uongozi wa klabu hiyo kukataa.

Kichuya ni miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wanacheza kwa kiwango kizuri na kuisaidia timu yake hiyo, jambo ambalo timu nyingi zimekuwa zikimnyemelea.

Kwa mujibu wa Gazeti la Championi, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amesemaa kuwa, dili lao na Ismailia juu ya Kichuya limekufa rasmi, lakini mchezaji huyo bado yuko sokoni kwa timu yoyote itakayomhitaji.

“Ile dili kati yetu na Ismailia ilishakufa rasmi kwa sasa hakuna ishu ya Kichuya kwenda huko, lakini tupo tayari kupokea ofa yoyote ile, iwapo kuna timu itamhitaji tutakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo.

“Simba tumekuwa na desturi ya kuwaachia wachezaji wetu kuwauza pale tunapofanikiwa kupata timu ya kucheza, hivyo mchezaji yeyote yule atakayetakiwa tutakuwa tayari kumuachia,” alisema Manara.
Kichuya awekwa sokoni Kichuya awekwa sokoni Reviewed by Zero Degree on 10/23/2017 11:01:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.