Loading...

Mashabiki wamwandama Bakayoko kwa kutotimiza alichoahidi


Akizungumza na waandishi wa habari kabla ya mechi ya Crystal Palace dhidi ya Chelsea, Timoue Bakayoko aliahidi kitu kwa mashabiki.

Bakayoko aliahidi kufanya mabadiliko makubwa ya muonekano wa nywele zake atakapofungua ukurasa wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Kwa mujibu wa taarifa ya 'The Sun', Bakayoko alisema: "Nikifanikiwa kufunga goli nitabadilisha rangi ya nywele zangu kuwa bluu au rangi nyingine."

"Huwa napendelea kubadili rangi ya nywele zangu mara kwa mara, na imekua inaniletea bahati nzuri. Tangu tulipocheza na Manchester City niliweka rangi nyeupe."


Hata hivyo, hadi kufikia jana Jumamosi, Chelsea ilipoibuka kidedea kwa ushindi wa bao 4-2 dhidi ya Watford, Bakayoko aliendelea kuonekana na nywele zenye rangi nyeupe.

Jambo hilo limeoneka kutowafurahisha mashabiki, ambao tayari wameanza kutoa malalamiko yao kwenye mitandao ya kijamii.

Tazama baadhi ya maoni yaliyotolewa na mashabiki hapo chini:


Mashabiki wamwandama Bakayoko kwa kutotimiza alichoahidi Mashabiki wamwandama Bakayoko kwa kutotimiza alichoahidi Reviewed by Zero Degree on 10/22/2017 11:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.