Rais Mugabe avuliwa cheo
"Nimesikiliza vizuri wale wote ambao wameelezea hisia zao," mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema katika taarifa.
Awali alikuwa ameisifu Zimbabwe kwa kujitolea kuboresha afya ya umma.
Lakini wakosoaji walisema kuwa mifumo ya afya nchini Zimbabwe iliporomoka chini ya utawala wa Mugabe wa miaka 30.
Wafanyakazi mara nyingi hukosa kulipwa na wakati mwingine dawa hukosekana huku Mugabe mwenyewe akisafiri nje ya nchi kupata matibabu.
Bw. Tedros alisema ameongea na serikali ya Zimbabwe na kuamua kuwa, suala la kumvua Mugabe wadhifa huo ni kwa manufaa ya WHO.
Alisema anasalia kujitolea kufanya kazi na chi zote na viongozi wake kujenga huduma bora za afya.
Uteuzi wa Bw. Mugabe ulipingwa vikali, kati ya wale ambao walikosoa uamuzi huo ni pamoja na Serikali ya Uingereza, waziri mkuu wa Canada na mashirika mengine kadha pamoja na watumiaji wa mitandao ya kijamii.
Kufuatia kukosolewa kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu na kushangazwa kwa mataifa mengi wanachama, WHO haikuwa na lingine ila kufuata mpango wake wa kumvua Robert Mugabe wadhifa wa balozi wa nia njema.
Rais Mugabe avuliwa cheo
Reviewed by Zero Degree
on
10/23/2017 12:34:00 AM
Rating: