Loading...

Mganga atiwa mbaroni kwa tuhuma ya kubaka watoto 14


Jeshi la polisi mkoani Singida linamshikilia mganga wa kienyeji mkazi wa mtaa wa Minga kata Mitunduruni mjini hapa, Daud Idd (74) kwa tuhuma ya kubaka watoto 14 wenye umri kati ya miaka saba na 12 na kuwasababishia maumivu makali katika sehemu zao za siri.

Babu Karatu imeelezwa kuwa alikuwa akishirikiana kutenda vitendo hivyo na mtoto wa mdogo wake dereva Abdallah Kola (31).

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Kamanda Jeshi la Polisi mkoani hapa, SSP Isaya Mbughi, alisema mtuhumiwa inadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Desemba mwaka jana, hadi Oktoba mwaka huu.

Akifafanua, alisema kuwa mwathiriki mmoja (jina tunalo) mwenye umri wa miaka saba, Oktoba 16 mwaka huu saa 11.45 jioni wakati akiogeshwa na mama yake, alilalamika kuwa anasikia maumivu makali katika sehemu yake ya siri.

Alisema baada ya binti kuyo kulalamika kwa mama yake, mama huyo aliweza kumchunguza kwenye sehemu zake za siri,na kubaini kuwa michumbuko katika sehemu yake ya siri inayotokana na kuingiliwa kimwili.

“Mama huyo baada ya kuona michumbuko hiyo kwenye sehemu za siri za binti yake, alimhoji mtoto wake na mtoto huyo aliweza kumtaja mganga wa kienyeji Karatu. Mwaathirika huyo alienda mbele zaidi na kumweleza mama yake kuwa si yeye pekee kufanyiwa vitendo hivyo, bali wapo watoto wengi wamefanyiwa vitendo hivyo,” alifafanua zaidi Mbughi.

Kaimu kamanda huyo, alisema baada ya hapo mama huyo alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa wa Minga,na kisha yeye na mwenyekiti wa mtaa waliweza kuongozana hadi kituo cha kati cha polisi mjini hapa.

“Jeshi la Polisi liliweza kuwakamata watuhumiwa hao ambao wanaishi katika nyumba moja kwa tuhuma ya ubakaji. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa watoto waliofanyiwa unyama huo, wanasoma katika shule za msingi Singidani, Nyerere na Mughanga,” alisema.

SSP Mbughi alisema mbinu iliyokuwa inatumika kuwanasa watoto hao wa kike, ni kuwarubuni na kasha kuwaonyesha video/movie, kwenye kompyuta mpakato.

“Wakati watoto hao wa kike wakiendelea kuangalia video sembuleni, mtuhumiwa huyo Babu , alikuwa akichomoa mmoja na kuingia naye chumbani na kumwingilia kimwli.Wachache alikuwa akiwachezea sehemu zao za siri.Baada kuingiliwa kimwili,watoto hao walikuwa wakipewa zawadi ya shilingi mia mbili au shilingi 2,000,” alisema na kuongeza.

“Watoto hawa wa kike,walijenga mazoea ambapo kila inapofika muda wa mapumziko na muda wa mchana baada ya kuruhusiwa kwenda nyumbani, hupitia nyumbani kwa watuhumiwa kwa lengo la kungalia video kwa mganga wa kienyeji. Mganga huyo na mtoto wa mdogo wake, walikuwa wakitumia mwanya huo kutekeleza ukatili huo”.

Kaimu kamanda huyo,alisema watuhumiwa baada ya kumaliza kufanya vitendo hivyo, mganga wa kienyeji Karatu Babu,alikuwa akiwapaka unga kwenye paji la uso, na kuwatisha kuwa wathubutu kusema kwa mtu ye yote juu ya vitendo hivyo,ni lazima watakufa.

“Jeshi la polisi lilifika katika shuel husika na kufanikiwa kuwapata watot 14 wanaosadikiwa kubakwa na watuhumiwa.Watoto hao walifanyiwa vipimo na daktari katika hospitali ya mkoa,na 12 walibainika kuingiliwa kimwili. Hata hivyo,idadi inaweza kuongezeka kwa sababu bado daktari ataendelea kuwafanyia vipimo wanafunzi zaidi,” alisema Mbughi.

Alisema kwa sasa bado wanaendelea na mahojiano na watuhumiwa na mara utakapomalizika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma ya ubakaji inayowakabili.
Mganga atiwa mbaroni kwa tuhuma ya kubaka watoto 14 Mganga atiwa mbaroni kwa tuhuma ya kubaka watoto 14 Reviewed by Zero Degree on 10/22/2017 12:48:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.