Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 23 Octoba, 2017


Jurgen Klopp amekiri kwamba Liverpool inaweza kukosa kwenye nne bora, na amewatupia lawama wachezaji wake kufuatia kichapo cha goli 4-1 dhidi ya Tottenham. (Daily Mail)

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anataka kutumia mtaji alioupata baada ya kumuuza Diego Costa kumnasa mshambuliaji wa Real Madrid, Gareth Bale.

Kobe Bryant anadai Harry Kane anaweza kuja kufikia ubora wa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Andrew Surman anahisi ushindi wa Bournemouth dhidi ya klabu ya Stoke City umerejesha heshima yao. (Daily Star)

Alan Shearer anasema Newcastle inaweza kuwa na matumaini mapya kamaMike Ashley sells ataiuza klabu hiyo, na kudai kwamba litakuwa ni jambo zuri sana kwa Rafael Benitez. (Sun)

Antonio Conte asisitiza kutokuwa na hofu ya kupoteza kibarua chake Chelsea, akidai kwamba yeye yuko tofauti na makocha wengine waliotangulia.

Rob Elliot anasema kwamba, wachezaji wa Newcastle wanashauku ya kupata mmiliki mpya wa klabu atayeleta mafanikio. (Daily Mirror)

Bernardo Silva anaweza kuwa mchezaji wa kwanza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza kuadhibiwa na FA kwa kujiangusha mchezoni. 
(Express)

Mark Hughes amekana kuwepo kwa mgomo ndani ya klabu ya Stoke City kufuatia matokeo mabovu waliyopata hivi karibuni.

Sean Dyche anasema anahofia kuporomoka kwa maadili mchezoni baada ya Bernardo Silva kufanikiwa kujiangusha uwanjani na kupewa penati dhidi ya Burnley. (Telegraph)

Ronald Koeman anasisitiza kwamba yeye peke yake ndiye anayeweza kuinusuru Everton kwenye Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu, baada ya kichapo cha goli 5-2 dhidi ya Arsenal. (Gaurdian)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 23 Octoba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 23 Octoba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 10/23/2017 10:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.