CHADEMA yatangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Songea Mjini
Mwenyekiti wa Chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA mkoa wa Ruvuma Bw. Erenius Ngwatura amesema wanaunga mkono tamko lililotolewa na Mwenyekiti wao wa taifa wa CHADEMA Mheshimiwa Freeman Mbowe na kubainisha kuwa uchaguzi wa udiwani uliopita kwa kata 43 uligubikwa na dosari kadhaa.
Kaimu Katibu wa CHADEMA jimbo la Songea mjini Bw.Masumbuko Mbogoro ansema sababu nyingine ya wao kujitoa kushiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Songea mjini ni kutokana na maombi yao kwa tume ya uchaguzi ya kutaka uchaguzi usogezwe mbele kutosikilizwa.
Source: ITV
CHADEMA yatangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Songea Mjini
Reviewed by Zero Degree
on
12/13/2017 12:28:00 PM
Rating: