Zitto Kabwe, Hussein Bashe waungana kulaani kitendo cha Serikali kuhoji uraia wa Askofu Niwemugizi
Wabunge hao kwa nyakati tofauti wameeleza hisia zao juu ya jambo hilo na kudai watu wanaofanya jambo hili ni wazi hawana hofu ya Mungu lakini pia ni njia ya kuwatisha watu hususani wale ambao wanakuwa wanaikosoa serikali.
Hata hivyo Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe naye amechangia na kusema kuwa suala la Uraia hutumika kama silaha dhidi ya watu ambao wanaonekana kuikosoa Serikali kwa mambo mbalimbali ambayo serikali inakuwa inafanya.
Askofu Severine Niwemugizi amesema kuwa amehojiwa kuhusu uraia wake mara mbili. Mara ya kwanza aliitwa kwenye ofisi za uhamiaji Ngara Novemba 28, 2017 na mara ya pili Disemba 4, 2017.
"Najuai inavyokuwa unapoambiwa ama kuanza kujazishwa fomu na kuhojiwa juu ya Uraia Wako ni kama kujazishwa fomu kuambiwa huyu sio Mama yako or Baba yako. Pole Askofu Severine Niwemugizi wanaofanya haya hawana hata hofu ya Mungu" aliandika Hussein Bashe.
Hata hivyo Mbunge wa Kigoma Mjini Mhe. Zitto Kabwe naye amechangia na kusema kuwa suala la Uraia hutumika kama silaha dhidi ya watu ambao wanaonekana kuikosoa Serikali kwa mambo mbalimbali ambayo serikali inakuwa inafanya.
"Baba askofu pole sana. Kuna watu wakubwa tu kwenye Taasisi nyeti wanaamini kwa ushahidi kuwa aliyeagiza uhojiwe mwenyewe sio raia wa Tanzania. Suala la Uraia hutumika kama silaha dhidi ya wakosoaji wa Serikali. Ni ushamba" alisisitiza Zitto Kabwe.
Askofu Severine Niwemugizi amesema kuwa amehojiwa kuhusu uraia wake mara mbili. Mara ya kwanza aliitwa kwenye ofisi za uhamiaji Ngara Novemba 28, 2017 na mara ya pili Disemba 4, 2017.
Zitto Kabwe, Hussein Bashe waungana kulaani kitendo cha Serikali kuhoji uraia wa Askofu Niwemugizi
Reviewed by Zero Degree
on
12/13/2017 12:18:00 PM
Rating: