Loading...

Kheri James atangazwa kuwa mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa

Kheri James
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, ambaye pia ni mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa (UVCCM), leo amemtangaza Kheri James kuwa Mwenyekiti mpya atakayeongoza kwa miaka mitano.

Kheri ametangazwa mshindi baada ya kupata Kura 319 kati ya kura 583 zilizopigwa akiwashinda wenzake 6 aliokuwa akichuana nao kuwania nafasi hiyo. Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imechukuliwa na Tabia Mwita.

Mkutano wa Uchaguzi wa UVCCM umefanyika mjini Dodoma kwenye ukumbi wa Chuo Cha Mipango. Mbali na wajumbe wa idara hiyo ya vijana wengine walioshuhudia kutangazwa kwa Kheri ni Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana.

Mkutano huo wa uchaguzi wa UVCCM ulifunguliwa jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Magufuli na unafungwa leo na Rais wa Zanziobar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.

Wagombea na Kura walizopata:
  1. Kheri James - kura 319
  2. Tobias Mwesiga - kura 127
  3. Simon Kipala - kura 67
  4. Kamana Juma - kura 27
  5. Juma Mwaipaja - kura 19
  6. Seif Mtoro - kura 16
  7. Mganwa Nzota - kura 1
Kheri James atangazwa kuwa mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa Kheri James atangazwa kuwa mwenyekiti mpya wa UVCCM Taifa Reviewed by Zero Degree on 12/11/2017 04:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.