Jibu la Hazard baada ya kuulizwa kama anahofia kupangwa na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa
Eden Hazard akishangilia bao |
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza wamepangwa na vigogo hao wa Catalonia kwenye droo iliyofanywa leo Jumatatu, na mchezo wa pili kuchezwa katika dimba la Nou Camp.
Lakini wakati akizungumza na 'BT Sport' baada ya sare ya goli 1-1 na Atletico Madrid katika mechi ya mwisho kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Jumanne iliyopita, Mbelgiji huyo hakuonyesha hofu ya kuwepo kwa uwezekano wa kumkabili Lionel Messi na wengineo.
Mchezo wa kwanza utachezwa Magharibi ya jiji la London mwezi Februari na wa mwisho utachezwa Catalonia mwezi Machi.
Lionel Messi, Suarez wakishangilia bao katika mechi yao dhidi ya Villareal |
"Hilo sio tatizo, sisi ndio Chelsea!" Hazard alimwambia mwandishi baada ya mechi hiyo iliyochezewa Stamford Bridge.
"Timu yetu ni kubwa, hivyo tunaweza kupambana na yeyote.
"Tunatambua kwamba PSG na Barcelona ni timu nzuri sana, lakini sisi ni Chelsea, hivyo tunatakiwa kuwa tayari kwa kila kitu."
Akionyesha kufurahishwa na kujiamini kwa Hazard, mwandishi alimuuliza hivi: "Unajipa nafasi ya kusonga mbele zaidi, sio?"
Kisha Hazard alijibu: "Ndio! Tunaweza kufanya kila kitu!"
Mchezo wa kwanza utachezwa Magharibi ya jiji la London mwezi Februari na wa mwisho utachezwa Catalonia mwezi Machi.
Jibu la Hazard baada ya kuulizwa kama anahofia kupangwa na Barcelona kwenye Ligi ya Mabingwa
Reviewed by Zero Degree
on
12/11/2017 03:55:00 PM
Rating: