Loading...

Droo kamili ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora


Chelsea wamepangwa kukutana na Barcelona hatua ya 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, Tottenham nao wakapewa mabingwa wa Italia Juventus baada ya droo kufanywa.

Viongozi wa Ligi Kuu ya uingereza, Manchester City watakutana na FC Basel ya Uswizi, Manchester United watakutana na Sevilla inayocheza Ligi ya La Liga nao Liverpool watakutana na FC Porto ya Ureno.

Mabingwa watetezi Real Madrid wamepangwa kukutana na Paris St-Germain.

Klabu tano kutoka Ligi Kuu ya Uingereza zilifuzu kwa hatua ya makundi msimu huu, ambapo ilikuwa ni rekodi katika historia ya ligi hiyo.

Chelsea ndio klabu pekee ya Uingereza iliyofuzu kuingia katika hatua ya 16 bora ikiwa katika nafasi ya pili kutoka kundi lao, wakati klabu nyingine zote zikimaliza kileleni.

Washindi wa makundi watakuwa ugenini mechi za kwanza tarehe 13/14 na 20/21 Februari na nyumbani mechi za marudiano mnamo tarehe 6/7 na 13/14 Machi.

Fainali itachezewa Kiev mnamo tarehe 26 Mei.

Droo kamili: Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
  • Juventus v Tottenham
  • FC Basel v Manchester City
  • Porto v Liverpool
  • Sevilla v Manchester United
  • Real Madrid v PSG
  • Shakhtar Donetsk v Roma
  • Chelsea v Barcelona
  • Bayern Munich v Beskitas

Droo kamili ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora Droo kamili ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora Reviewed by Zero Degree on 12/11/2017 03:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.