Loading...

Kauli ya Kocha Ernesto Valverde kuhusu Messi baada ya Barcelona kushinda goli 6-1


Ernesto Valverde amemtaja Lionel Messi kama mchezaji mwenye uwezo wa pekee zaidi, ingawa kitendo cha kufunga magoli manne kwenye mchezo mmoja linaonekana ni suala la kawaida kwa meneja huyo.

Nyota huyo wa Argentina alionyesha uwezo wake kwenye La Liga pale Barcelona ilipoichakaza Eibar kichapo cha goli 6-1 siku ya Jumanne, na sasa anatimiza magoli 11 kwenye michezo yake mitano aliyoshiriki katika michuano yote.

Pamoja na mchezaji aliyesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha, Ousmane Dembele kuwa benchi kwa sababu ya majeraha aliyopata hivi karibuni na Luis Suarez kutocheza pia, Messi alisimama kuibeba timu yake, kitu ambacho kimemfanya kocha Valverde amwagie sifa za kutosha.

"yuko kati ya wachezaji wenye uwezo mkubwa zaidi uwanjani ambao nimeshawahi kukutana nao maishani mwangu. Namaanisha ni zaidi yao," alisema.

"Kutoka kwenye hali ambayo, hakuna kitu chochote kinachotegemewa kutokea, anaweza akatufanyia mambo mazuri na mabaya kwa maadui.

"Yeye kufunga magoli manne ni suala la kawaida kwake. Amefanya hivyo mara ngingi, katika mechi nyingi na sehemu nyingi, suala hilo hujirudia mara nyingi."


Messi alifungua ukurasa wa magoli kwa kufunga bao mnamo dakika ya 20 kwa mpira wa adhabu kabla ya kuonyesha umahili wa kumalizia alipopachika bao akipokea akisaidiwa na Paulinho dakika kadhaa zilizofuata na kufanikiwa kupata 'hat-trick' nyingine.

Barcelona walimalizia kuseleka nyavuni mnamo dakika ya 87 pale Messi alipo kwamisha mpira wavuni kwa kumalizia pasi iliyotoka kwa Aleix Vidal.

Licha ya kumpoteza Neymar aliyetimkia PSG, maumivu yote yaliyopelekea hadi uongozi wa rais wa Barcelona, 
Josep Maria Bartomeu kuhojiwa, juhudi za Messi zimeiweka Barcelona juu kwenye msimamo wa ligi.
Kauli ya Kocha Ernesto Valverde kuhusu Messi baada ya Barcelona kushinda goli 6-1 Kauli ya Kocha Ernesto Valverde kuhusu Messi baada ya Barcelona kushinda goli 6-1 Reviewed by Zero Degree on 9/20/2017 06:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.