Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 21 Februari, 2018

Willian
Wiliian ana amini kuwa kiwango alichokionyesha katika mechi ya Klabu Bingwa kati ya Chelsea na Barcelona kilikuwa ni moja ya viwango vyake bora kwa klabu yake.

Klabu ya Liverpool ni miongoni mwa vilabu vinavyohitaji saini ya golikipa namba moja wa Roma, Alisson Becker.

Marcus Rashford anaweza kulazimika kuondoka Manchester United ili apate nafasi ya mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza, kwa mujibu wa Dennis Wise. (Sky Sports)

Klabu ya Chelsea inakabiliana na ushindani mkubwa kutoka klabu ya Bayern Munich katika kuwania saini ya winga wa Borussia Dortmund, Christian Pulisic anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 88.

Barcelona imeipiku Manchester United katika kumsajili kiungo Gremio na Timu ya Taifa ya Brazil, Arthur Melo.

Klabu ya Wigan imesistiza kuwa mbinu zao za ulinzi zilikuwa zinakubalika wakati wa mechi ya michuani ya FA dhidi ya Manchester City. (Daily Mail)

Manchester City imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Liverpool, Emre Can.

Marco Asensio
Kiungo wa klabu ya Real Madrid, Marco Asensio amesema kuwa alipata ofa kutoka klabu tano, zikiwemo Liverpool, Chelsea, na Arsenal.
 
Idrissa Gueye amesaini mkataba mpya na klabu ya Everton, ambao utaisha mwaka 2022. (talkSport)

Aaron Ramsey ana wakati mgumu kujiweka fiti kwa ajili ya mechi ya fainali ya michuano ya Carabao kati ya Arsenal na Manchester City. (Telegraph)

Jorginho anaweza kuruhusiwa aondoke Napoli - kufungua milango kwa klabu ya  Manchester United inayomtaka nyota huyo.

Klabu ya Arsenal inatazamia kumsajili beki wa Juventus na Timu ya Taifa ya Italia, Daniele Rugani.

Leo Ulloa anataka kurejea moja kwa moja katika klabu ya Brighton na binafsi anatambua kuwa kuisaidia klabu hiyo kusalia juu ni zaidi ya kushinda taji.

Golikipa wa klabu ya Burnley, Tom Heaton alirejea uwanja baada ya miezi mitano katika mechi isiyokuwa na mashabiki - lakini alisababisha penalti ndani ya sekunde 60.

Jamie Vardy hataki kukubaliana na suala la kumwacha Harry Kane atawale nafasi ya mshambuliaji kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Uingereza kitakachoshiriki Kombe la Dunia.

Robert Pires
Robert Pires anasema kuwa Kombe la Europa ndio nafasi pekee kwa klabu ya Arsenal kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa msimu wa 2018/19. (Sun)

Kocha wa Timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amesema kuwa Oliver Giroud alifanya vizuri kuondoka Arsenal kwenda Chelsea mwezi Januari.

Crystal Palace imejiandaa kumsajili golikipa wa zamani wa klabu ya Liverpool na Timu ya Taifa ya Brazil, Diego Cavalieri kama mchezaji huru.

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesema kuwa hahofii kufukuzwa kazi katika klabu hiyo. (ESPN)

Kiungo wa klabu ya Watford, Abdoulaye Doucoure amedai kuwa Arsenal, Liverpool na Tottenham zinataka kumsajili.

Beki wa klabu ya Lazio, Stefan de Vrij, ambaye mkataba wake unaelekea ukingoni ana matamanio ya kujiunga na Manchester United. (Mirror)

Jose Mourinho anatarajia kumkaribisha Paul Pogba kikosini lakini amemuonya kuwa hawezi kumhakikishia nafasi ya kudumu kikosini.

David Moyes amesema kuwa ataendelea kuwa meneja wa klabu ya West Ham, huku akiendelea kutazamia kibarua chenye maslahi mazuri zaidi. (Express)

Manchester United iko tayari kushindana na klabu ya Real Madrid kuwania saini ya mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icardi.

Isaac Christie-Davies
QPR iko inamchunguza chipukizi wa klabu ya Chelsea, Isaac Christie-Davies kwenye muda wa majaribio. (Star)

Kiungo wa klabu ya Fulham, Kevin McDonald amemtaka meneja wa Timu ya Taifa ya Uskoti, Alex McLeish amchague yeye. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 21 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 21 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/21/2018 11:38:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.