Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 12 Decemba, 2017
Jack Wilshere |
Arsenal wataanzisha mkakati wa mwisho kujaribu kumshawishi Mesut Ozil asaini mkataba npya, huku zikiwa zimebaki wiki tatu pekee kabla ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili mwezi Januari.
Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte ana presha mpya kufuatia mabadiliko katika ngazi za kiutawala za klabu hiyo.
Crystal Palace inajiamini kuwa inaweza kufanikiwa kumnasa golikipa wa klabu ya Espanyol, Diego Lopez. (Mirror)
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Olivier Giroud amesema kwamba ataamua kuhusu future yake mwezi Januari akitazamia kuzifanya ndoto zake za kucheza kombe la dunia kuwa hai.
Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Olivier Giroud amesema kwamba ataamua kuhusu future yake mwezi Januari akitazamia kuzifanya ndoto zake za kucheza kombe la dunia kuwa hai.
Real Madrid watafanya uamuzi juu ya kumshawishi golikipa wa Chelsea, Thibaut Courtois atue Bernabeu mwezi huu.
Ki Sung-yueng |
Kiungo wa klabu ya Swansea, Ki Sung-yueng ataweka kando mazungumzo ya mkataba mpya lengo likiwa ni kuipigania klabu isishuke daraja. (Sun)
Sam Allardyce atafanya mazungumzo ya ana kwa ana na wachezaji wa Everton na kutoa wito kwamba wanatakiwa wawe waaminifu akiwa katika mikakati ya kusafisha kikosi chake.
Sam Allardyce atafanya mazungumzo ya ana kwa ana na wachezaji wa Everton na kutoa wito kwamba wanatakiwa wawe waaminifu akiwa katika mikakati ya kusafisha kikosi chake.
Charlie Austin ameibiwa siri na mchezaji mwenzake wa Southampton, Oriol Romeu kwamba atajumuishwa katika kikosi cha Timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia. (Daily Mail)
Gareth Bale |
Manchester United na Tottenham ziko kwenye ushindani mkubwa kuwania saini ya nyota wa klabu ya Real Madrid, Gareth Bale. (Star)
Mshambuliaji wa Manchester united, Romelu Lukaku alituhumiwa kucheza kama mchezaji wa rugby alipokuwa akijaribu kuwakabili wachezaji wa Manchester City katika mechi baina ya mahasimu hao wawili wa Manchester uliochezwa Jumapili.

Mark Hughes ana kibarua kizito katika mechi zake mbili zinazofuata akipigania kutetea nafasi yake katika klabu ya Stoke City.
Christian Benteke baada ya kukosa penati dhidi ya Bournemouth |
Roy Hodgson anasema kwamba Christian Benteke lazima awaombe msamaha mashabiki wa Crystal Palace baada ya kufanikiwa kuelewana na meneja pamoja na wachezaji wenzake kufuatia kukosa penati wikendi iliyopita. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 12 Decemba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
12/12/2017 11:27:00 AM
Rating: