Loading...

Ajali ya basi la abiria yaua na kujeruhi mkoani Kagera


BASI la abiria Kampuni ya Fikoshi Investment linayofanya safari zake kati ya Kaisho, Bukoba na jijini Mwanza limepata ajali katika eneo la Nkwenda Wilayani Kyerwa mkoani Kagera na kusababisha kifo cha kondakta wa basi hilo.


Kondakta wa basi hilo ambaye bado hajafahamika jina lake, alifariki papo hapo, huku majeruhi kadhaa wamekimbizwa katika Hospitali teule ya Nyakahanga na wengine katika Kituo cha Afya Nkwenda kilicho karibu na eneo la ajali.
Ajali ya basi la abiria yaua na kujeruhi mkoani Kagera Ajali ya basi la abiria yaua na kujeruhi mkoani Kagera Reviewed by Zero Degree on 2/24/2018 09:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.