Loading...

Mabomu yaliotegwa ndani ya magari yaua watu 38 nchini Somalia

Shambulio hilo lilidaiwa kutekelezwa na al-shabab
Mabomu mawili yaliotegwa ndani ya magari mawili yamewaua watu 38 katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, kulinagana na maafisa.

Bomu la kwanza lilitokea nje ya jumba la rais siku ya Ijumaa huku la pili likilipuka katika hoteli moja ilio karibu .

Makumi ya watu wamejeruhiwa. Kundi la al-Shabab ambalo limekuwa likijaribu kupindua serikali ya Somalia limekiri kutekeleza shambulio hilo.

Ufyatulianaji wa risasi ulifuatia baadaye karibu na ikulu ya rais ambapo washambuliaji watano waliuawa.

Mabomu hayo ya Ijumaa ndio ya hivi karibuni katika msururu wa mashambulio yanayotekelezwa na al-Shabab, kundi ambalo lilidhibiti Mogadishu kabla ya kufurushwa na wanajeshi wa muungano wa Afrika 2011.

Mnamo mwezi Oktoba, zaidi ya watu 500 waliuawa katika bomu lililotegwa ndani ya lori mjini humo.

Maafisa walilaumu al-shabab lakini kundi hilo halikusema kwamba lilihusika.

Kisa hicho cha hivi karibuni kilianza wakati gari lilipokataa kusimama katika kizuizi nje ya jumba hilo la rais kabla ya kulipuliwa, vyombo vya habari vinasema.

Hili lilifuatiwa na ufyatulianaji wa risasi kati ya wapiganaji na vikosi vya usalama. Baadaye gari lililokuwa limeegeshwa karibu na hoteli lilipuka .

Hatahivyo al-shabab lilisema kuwa lilikuwa likiwalenga maafisa wa kijeshi.

Kundi hilo lilisema kuwa wapiganaji watano wakiwemo madereva wawili walifariki huku wanajeshi 35 pia wakiuawa.

Msemaji wa polisi aliambia chombo cha habaricha reuters kwamba kulikuwa na wanajeshi wengi waliolinda barabara hiyo iliokuwa ikielekea katika makao ya rais.
Mabomu yaliotegwa ndani ya magari yaua watu 38 nchini Somalia Mabomu yaliotegwa ndani ya magari yaua watu 38 nchini Somalia Reviewed by Zero Degree on 2/24/2018 08:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.