Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 24 Februari, 2018

Nemanja Matic
Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anajuta kumruhusu Nemanja Matic aondoke Stamford Bridge kwenda Manchester United.


Charlie Nicholas anadai kuwa mtindo wa mchezo wa klabu ya Manchester United umebadilika tangu kuwasili kwa Alexis Sanchez.

Beki wa klabu ya Tottenham, Jan Vertonghen anaweza kucheza soka hadi akiwa katika umri wa miaka 40, kwa mujibu wa Mauricio Pochettino. (Sky Sports)

Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola amekubali kusaini mkataba  mpya na klabu hiyo wenye thamani ya takriban pauni milioni 20 kwa mwaka,  ambao utaisha mwaka 2021. (Daily Mail)

Real Madrid inamfuatilia Raheem Sterling kwa karibu zaidi, huku kukiwa na sintofahamu juu ya hatima ya nyota huyo katika klabu ya Manchester City.

Klabu ya Tottenham iko tayari kumruhusu Toby Alderweireld aondoke kwenye majira ya joto. (talkSport)

Jean Michael Seri
Manchester United imeongeza juhudi katika mbio za kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Nice, Jean Michael Seri - sakata la Paul Pogba likizidi kushika kasi.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya AC Milan, Massimiliano Mirabelli anasema kuwa anaionea huruma klabu ya Arsenal baada ya kuwa imepangwa kukutana na vigogo hao wa Sirie A kwenye raundi ya 16 ya Europa Ligi.

David Ospina amesema kuwa atalazimika kuamua juu ya 'future' yake kwenye majira ya joto baada ya kudai kwamba anaumizwa na kitendo cha kuwa golikipa namba mbili wa klabu ya Arsenal.

Klabu ya Grimsby iko tayari kufanya mazungumzo na Sol Campbell kuhusiana na nafasi ya umeneja katika klabu hiyo. (Mirror)

Chelsea inakabiliana na upinzani kutoka PSG kwenye mbio za kuwania saini ya golikipa wa klabu ya AC Milan, Gianluigi Donnarumma.

Benjamin Mendy anatgemewa kurejea kwenye kikosi cha kwanza cha klabu ya Manchester City mwezi ujao.

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger anasema kuwa mafanikio ya klabu ya Manchester City hayahusiani kabisa na Pep Guardiola bali ni kiasi cha fedha anachotumia. (Sun)

Mino Raiola na Paul Pogba
Kitendo cha wakala wa Paul Pogba, 
Mino Raiola kulalamika kwamba Manchester United haimtendei haki mteja wake kinazidi kuichukiza klabu hiyo.

Arsenal inahofu kwamba Aaron Ramsey atajaribu kuchelewesha kutia saini kandarasi mpya na kurejesha hali ya taharuki kama ilivyokuwa kwa Mesut Ozil na Alexis Sanchez msimu huu.

Chelsea na Crystal Palace zimetofautiana juu ya matibabu ya Ruben Loftus-Cheek, ambaye amekuwa nje ya dimba kwa karibuni miezi miwili sasa kutokana na majeraha katika kifundo cha mguu. (Times)

Antonio Conte amesisitiza kwamba, huwa anatumia akili wakati anapoamua kumwacha Willian kwenye benchi. (Express)

Mauricio Pochettino amesema kuwa Tottenham inaweza kuendelea kuwa imara bila Toby Alderweireld.

Pep Guardiola hahofii hatua ambazo FA itachukua juu yake na anategemewa kuvaa utepe wa rangi ya njano kwenye fainali ya michuano ya Carabao katika dimba la Wembley. (Star)

Alan Pardew amekiri kwamba mstakabali wa maisha yake katika klabu ya West Brom uko shakani baada ya mechi 16 pekee kama meneja wa klabu hiyo.

Meneja wa klabu ya Everton, Sam Allardyce
Sam Allardyce ana matumaini ya kumaliza wasiwasi juu ya 'future' yake katika klabu ya Everton kwa kuiwezesha klabu hiyo kukaa kwenye nafasi ya kushiriki Ligi ya Europa kabla msimu huu haujaisha. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 24 Februari, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 24 Februari, 2018 Reviewed by Zero Degree on 2/24/2018 11:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.