Loading...

Arsenal kuzipiku Man United na Liverpool kumnasa nyota huyu wa Ligue 1

Kiungo wa klabu ya Nice, Jean Michael-Seri
Arsenal wanaripotiwa kuwa kwenye nafasi nzuri ya kushida mbio za kuwania saini ya kiungo wa Nice, Jean Michael-Seri mbele ya Manchester United na Liverpool kwa pauni milioni 35.

Seri ameonyesha kiwango cha kuvutia na kuingia kwenye orodha ya viungo wenye uwezo mkubwa kwenye Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) siku za hivi karibuni, inaonekana ni wazi kwamba Seri anaweza kuwa mtu sahihi kwa Arsenal, hivyo washika bunduki hao watakuwa na matumaini kwamba uvumi huo ni wa kweli.

Inadaiwa mkurugenzi wa Arsenal, Raul Sanllehi ana ukaribu mkubwa na wakala wa Seri kiasi cha kuipaklabu hiyo nafasi ya kushinda mbio hizo.

Awali, Seri alihusishwa na uhamisho kwenda Chelsea, Liverpool, Manchester United pamoja na Barcelona.

Thamani yake ya pauni milioni 35 inaweza kumfanya kuwa miongoni mwa wachezaji watakaolengwa na vilabu vingi kwenye usajili wa majira ya joto.
Arsenal kuzipiku Man United na Liverpool kumnasa nyota huyu wa Ligue 1 Arsenal kuzipiku Man United na Liverpool kumnasa nyota huyu wa Ligue 1 Reviewed by Zero Degree on 5/16/2018 01:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.